Takriban watu 143 wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko baada ya boti iliyokuwa imebeba mafuta kuwaka moto na kupinduka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa maafisa nchini humo.

Mkuu wa ujumbe wa wabunge wa kitaifa kutoka eneo kulikotokea ajali hiyo Josephine -Pacifique Lokumu ameeleza kuwa mamia ya abiria walikuwemo kwenye boti ya mbao kwenye Mto Kongo, kaskazini-magharibi mwa DRC siku ya Jumanne wakati moto huo ulipozuka.

Lokumu ameongeza kwamba “miili 131 ya kwanza ilipatikana siku ya Jumatano, huku mingine 12 ikiopolewa siku ya Alhamisi na Ijumaa. Miili hiyo ilikuwa imeteketea.

Hata hivyo, idadi kamili ya abiria waliokuwemo ndani ya boti hiyo bado haijajulikana japo duru zinasema boti hiyo ilikuwa imebeba mamia ya watu.