Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki Balozi John Ulanga ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na makumpuni ya Viet Nam, ambapo wamenadi fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zinazopatikana hapa nchini.
Mazungumzo na makumpuni hayo, yaliyofanyika jijini Ho Chi Minh, Mei 1, 2025 yalilenga kuyashawishi makapuni hayo kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi, uvuvi wa kisasa, kilimo na kutafuta soko la bidhaa za kilimo ikiwemo korosho.

Makampuni hayo yaliyotembelewa kwenye Makao Makuu ya Ofisi zao na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania ni pamoja na Viet Nam Association Seafood Exporters and Producers, Hao Binh Construction Cooperation na Viet Nam Cashew Association.
Viongozi na Watendaji Wakuu wa Makampuni hayo baada kuvutiwa na fursa na motisha zinazotolewa kwa wawekezaji nchini wameeleza utayari wao wa kuanza kufuata taratibu zitakazo wawezesha kufanya biashara na uwekezaji hapa nchini.
Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo hayo ulijumuisha Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Felista Rugambwa, Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji Bw. Vicent Minja, Mkurugenzi Mtendaji na Mmiliki wa Kampuni ya SM Holdings Bw. Nahdi Saleh Mbarak, ukiongozwa Balozi John Ulanga.



