Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Tabora
Mahakama ya Jakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora imewahukumu kifungo cha maisha jela baba na mtoto kwa kukutwa na hatia ya kusafirisha bangi kutoka Nzega Tabora na kuzipileka mkoani Shinyanga kinyume na sheria za nchi.
Familia hiyo ilitiwa hatiani jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi Wilaya ya Nzega mkoani hapa ,Saturini Mushi baada ya kuona washitakiwa kuwa na kosa na hujumu uchumi
Mushi aliwataja waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kuwa ni familia moja ambayo ni baba aliyetambulika kwa jina Ally Thabit (45) na mtoto Jonas Ally Thabiti (23) alisema kwa kifungo hicho kiwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya yaliyokatazwa kutokana na sheria za Tanzania.
Hakimu huyo alibainisha kwamba hukumu hiyo itakuwa ni mwanzo wa kukomesha vitendo vya kiulihalifu kwa wananchi kulima na kuunza bangi kinyume na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Awali Mwendesha Mashitaka kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Meshaki Lyabonge aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ya Wilaya ya Nzega mkonai Tabora kwamba mnamo Machi 13, mwaka jana katika msitu wa Mabatini, kijiji cha Kigandu Kata ya Mogwa wilayani humo watu hao wakiwa na pikipiki walikamatwa wakisafirisha bangi kilo 398 kwenye magunia wakipeleka mkoani Shinyanga
Mwendesha mashitaka huyo aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iliwe fundisho kwa walimaji wengine wa mazao ya aina hiyo nchini na kutaja kesi namba ya 7152 ya mwaka 2024.
Aidha washitakiwa hao waliomba kupunguziwa adhamu waliiambia Mahakama hiyo kwamba hilo ni kosa lao la kwanza hivyo wanaomba mahakama iwasemehe kwani hatarudia tena.
Hata hivyo hakimu hiyo alitupilia mbali ombi hilo na kutamka kifungo cha maisha jela na kupatiwa muda wa kakata rufaa kama hawakuridhika na hukumu hiyo.
