Moshi mweupe umeonekana ukifuka kutoka kwenye bomba la moshi katika Kanisa la Sistine Chapel, ni wazi mchakato wa upigaji kura umekamilika na makadinali wamemchagua mrithi wa Papa Francis.

Bado hatujui ni nani amechaguliwa, lakini itaonekana wazi watakapotokea kwenye roshani ya Kanisa la Sistine, ndani ya kama saa moja.

Umati wa watu unaimba “Viva papa”, ambayo ina maana ya “maisha marefu Papa” kwa Kiitaliano.

Muziki unaendelea kuchezwa kutoka kwa bendi ambayo sasa iko chini ya roshani katika uwanja wa St Peter’s Square.