Rais Samia Suluhu Hassan, amempongeza Profesa Mohamed Yakub Janabi kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kipindi cha 2025–2030.
Kupitia ujumbe wake rasmi, Rais Samia amesema ana imani thabiti kwamba uzoefu wa Profesa Janabi katika sekta ya afya utaleta mwelekeo mpya na mafanikio kwa bara la Afrika. “Una kila sifa ya kulitumikia bara letu na kuliongoza katika mafanikio makubwa zaidi,” amesema Rais Samia.
Ameishukuru pia jumuiya ya kimataifa na nchi wanachama wa WHO waliomuunga mkono Profesa Janabi, akisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za kuimarisha afya barani Afrika.
