

Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu tayari amepandishwa kizimbani leo Mei 19, 2025 kwa ajili ya kusubiri kutajwa kwa kesi mbili za jinai zinazomkabili ikiwemo uhaini na kuchapisha taarifa za uongo
Lissu anakabiliwa na kesi mbili zilizopo mbele ya mahakimu wawili tofauti huku kesi ya kuchapisha taarifa za uongo ikiwa imekamilika upelelezi na anatarajiwa kusomewa maelezo ya awali ‘Ph’.
Wanachama wa Chadema pamoja na viongozi mbalimbali wa Chadema akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, Godbless Lema, Jenerali Ulimwengu, Katibu Mkuu wa zamani wa chama hicho, Dkt Wilbroad Slaa wamejitokeza Mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo.


