Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameonyesha kughadhabishwa na ajali mbaya iliyotokea Jumatano wakati wa uzinduzi wa meli mpya ya kivita nchini humo akisema ni uzembe wa hali ya juu.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameitaja ajali hiyo kama ‘kitendo cha uhalifu’ ambacho hakingeweza kuvumiliwa.

Shirika la habari la serikali, KCNA limesema kuwa Kim aliyehudhuria hafla ya uzinduzi, amekosoa vikali ajali hiyo akisema imetokana na ‘uzembe’ na kuitia doa heshima ya nchi na kuamuru itengenezwe kabla ya mkutano mkuu wa chama tawala mwezi Juni.

Meli hiyo ya kijeshi ya tani 5,000 ni nyingine kubwa zaidi kuzinduliwa nchini Korea Kaskazini kwa mwaka huu, baada ya meli nyingine ya kijeshi yenye ukubwa kama huo kuzinduliwa mnamo mwezi Aprili.