Na Mwandishi Wetu

Mradi wa kituo cha umahiri wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu utasaidia kuwapa huduma watoto wachanga wenye changamoto ya upumuaji.

Mradi huo unatekelezwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS ) kwa kushirikiana na Serikali, na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDb).

Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya anayesimamia huduma za watoto wachanga, Felix Bundala alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi huo Kampasi ya Mloganzila Dar es Salaam.

“Serikali imeweka huduma madhubuti za watoto wachanga, lakini pia kuhakikisha vifo vinapungua,” amesema Bundala.

Alisema Serikali imenzisha wodi maalumu ya kulaza watoto wachanga kutoka hospitali 14 mwaka 2018 mpaka 318 mwaka 2025.

Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana, Brayson Kiwelu amesema wamefanikiwa kupunguza vifo vitolanavyo na uzazi kutoka vifo 556 kwa vizazi hai 100,000 hadi wastani wa vifo 104 kwa idadi hiyo.

Alisema licha ya juhudi za serikali, ila bado wanapambana kupunguza idadi iliyobaki huku akisema malengo ya dunia ni angalau vifo 12 kwa vizazi hai 1,000.

Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana, Brayson Kiwelu amesema wamefanikiwa kupunguza vifo vitolanavyo na uzazi kutoka vifo 556 kwa vizazi hai 100,000 hadi wastani wa vifo 104 kwa idadi hiyo.

Amesema licha ya juhudi za serikali, ila bado wanapambana kupunguza idadi iliyobaki huku akisema malengo ya dunia ni angalau vifo 12 kwa vizazi hai 1,000.

Aidha, Martha Mkoni Daktari Bingwa Bobezi wa watoto alisema vifo mara nyingi vinachangiwa na watoto kuzaliwa kabla ya muda wao, hivyo kupata tatizo la upumuaji.

“Kwa kipindi cha nyuma watoto walikuwa wakipumua wanashindwa kupatiwa msaada katika chumba cha kujifungulia, lakini wanapopewa rufaa katika hospitali kubwa namna ya kukuweka mtoto katika usalama ilikuwa ni changamoto,”

“Kwa hiyo mradi umekuja na ufumbuzi kwa kuangalia maeneo matatu, kwanza kumpa msaada pale anapozaliwa, pia kumuazishia matibabu ya upumuaji, atasafirishwa katika mfumo huo wa kupumua,” alisema daktari Mkoni.