Rais Yoweri Museveni na mkewe wameomba msamaha katika tukio ambalo ni nadra sana na kukubali kutokea kwa makosa ya hapa na pale katika mkutano uliofanyika uwanja wa Uhuru wa Kololo, viungani mwa jijini kuu la Kampala, Uganda.
Museveni na mkewe wamezungumza hayo wakiwa katika mkutano wa Injili, ambapo walisimama pamoja na kukiri kuwepo kwa mapungufu katika uongozi, kutokea kwa ufisadi, kujitenga kwa raia.
“Kama viongozi wakuu wa National Resistance Movement (NRM), tunawajibika kwa makosa yote tuliyofanya sisi wenyewe, mawakala wetu na wawakilishi wetu. Kwa hiyo, tunasimama hapa kutubu na kuomba radhi hasa wananchi wa Buganda na nchi nzima. Tunaomba urejesho na upendeleo.
Katika hotuba yake Rais Museveni alilipongeza kanisa kwa kile alichoeleza kuwa ni mabadiliko makubwa kutoka kuwa sehemu ya tatizo hadi sasa kuwa msingi wa amani, uwajibikaji na maendeleo ya kiroho nchini Uganda.
Mungu arejeshe neema ambayo tulikuwa nao mwanzoni na kutuunganisha tena kwa umoja wetu wa kitaifa na kujitolea kwa mabadiliko ya kijamii na uchumi wa nchi yetu pamoja, “viongozi hao wawili walisema katika taarifa yao ya pamoja.
Mkutano huo ulivutia maelfu ya waumini kutoka nchi nzima kwa sala, ibada, na wito mpya wa mabadiliko ya kitaifa kupitia imani.
