Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt Dorothy Gwajima amesema Wizara imetatua migogoro ya ndoa 97,234 hadi kufikia Aprili, 2025 kupitia Kitengo cha Ustawi wa Jamii katika ngazi ya Halmashauri hadi Taifa.
Amesema kati ya mashauri hayo mashauri 81,820 yalipatiwa ufumbuzi na mashauri 15,414 yalipelekwa mahakamani kwa hatua zaidi.
Waziri Gwajima ametoa kauli hiyo leo Mei 27,2025 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Amesema idadi ya ashauri yaliyopokelewa imeongezeka ikilinganishwa na mashauri 31,380 yaliyowasilishwa katika kipindi kama hiki cha mwaka 2023/2024 na ongezeko hili linatokana na kuongezeka kwa elimu kwa umma na uelewa wa jamii kuhusu kutoa taarifa za ukatili badala ya kuficha.
“Hatua hii imechangiwa na kuendelea kuimarika kwa huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii nchini, kuimarika kwa mifumo ya hamasa na utoaji wa taarifa katika jamii kupitia kampeni zinazotekelezwa,”amesema Waziri Gwajima.
