Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kukutana na marais wa Ukraine na Urusi nchini Uturuki baada ya pande hizo mbili kushindwa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alipendekeza kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin, na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakutane na Trump kwa raundi ya tatu baadaye mwezi huu, mjini Istanbul au Ankara.

Putin hadi sasa amekataa kushiriki katika mkutano wa ana kwa ana, lakini Zelensky amesema yuko tayari, akisisitiza kuwa masuala muhimu yanaweza kutatuliwa tu na viongozi.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, Trump yuko “tayari” kwa mkutano wa pande tatu ikiwa atalazimika kuhusishwa, lakini angetaka marais wa Ukraine na Urusi wakutane kwenye meza ya mazungumzo.