Watu kumi na sita walifariki dunia wakati wa maandamano ya kupinga serikali nchini Kenya Amnesty International imesema.

Maandamano hayo yalikuwa kumbukumbu ya mwaka mmoja kwa waliofariki wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha 2024 ambapo baadaye walivamia bunge.

Ikiwa si tofauti sana na kilichotokea mwaka jana, vijana walijitokeza kwa wingi wakiwa wamebeba bendera za Kenya, firimbi mabango na kuimba nyimbo za kupinga serikali.

Na muda si muda mchezo wa paka na panya ukashuhudiwa katika mitaa na miji mbalimbli nchini Kenya huku polisi wakikabili waandamanji kwa kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi.

Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Kenya (KNHCR), iliripoti katika mtandao wake wa X, kuwa zaidi ya 400 walijeruhiwa idadi hiyo ikijumuisha waandamanaji, maafisa wa polisi na wanahabari.