Wanajeshi wa DRC wamedungua ndege ya kusafirisha misaada ya kibinadam katika Mkoa wa Kivu ya Kusini

Ndege hiyo inaripotiwa kuwa ilikuwa ikielekea eneo la Minembwe kusafirisha dawa na chakula kwawaadhiriwa wa vita vinavyoendelea Mashariki mwa DRC.

Vugu vugu la AFC M23 limelaani shambulizi hilo ambalo limetokea chini ya saa 72 baada ya Kisainiwa kwa mkataba wa amani kati ya DRC na Rwanda mjini Washington.

Msemaji wa viguvugu hilo amesema kitendo hicho cha kikatili dhidi ya maafisa wa kusambaza misaada ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu na mkataba wa amani ulioidhinisha usitishwaji wa mapigano.

Jeshi la DRC limethibitisha kuwa lilidungua ndege moja ya kiraia ilioyokuwa katika anga yake. Kwa majibu wa taarifa iiyotolewa kupitia runinga ya taifa na msemaji wa jeshi Generali Sylvain Ekenge Ndege hiyo haikuwa na kibali kupaa katika anga zake

Watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wamefariki. Dawa na misaada ya chakula pia viliharibiwa.