NAla Ruja Masewa, JamhuriMedia, Mbeya
Mjumbe wa Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya MNEC Ndele Mwaselele, amekanusha Uvumi kwamba kuna mtia nia wa ubunge anambeba, na badala yake amejigamba kuwa yeye anatatua Kero za Wananchi na Kujenga ofisi za CCM kwenye wilaya zote.
Kauli ya MNEC-Ndele imekuja baada ya kuwepo kwa minong’ono na tetesi mitaani kwamba ametia nia ya kugombea ubunge kwenye Jimbo hilo, lakini baada ya kutoonekana akichukua fomu, wakamgeukia kwamba ana Mtia Nia anayembeba.
Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari jana (03/07/2025), Ndele amekanusha tetesi na minong’ono hiyo akidai;
Kazi ya MNEC si Kutuma watia nia wakagombee, si kuwa mgongoni mwao, isipokuwa kazi yangu ni kusikiliza Kero na kuhakikisha natimiza ahadi nilizoahidi, Kujenga Ofisi za CCM wilaya zote.
” Ni rai yangu Waandishi muelewe hakuna Kiongozi yeyote tangu Ngazi ya chini hadi taifa kwa Rais Samia Suluhu. aliyemtuma Mtu akagombee ili akae mngongoni mwake” alisema.
Amezitaja ofisi zilizojengwa kuwa ni za, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Ofisi ya Kyela na Ofisi ya CCM Mbalali, ambapo takribani zaidi ya sh. Milioni 10 ametumia kuwezesha kujenga na kuzikarabati ikiwemo kununua Mbao za kuezekea.

Ameonya ni rai yake “Watu wasitumie vibaya majina ya viongozi wa Klkitaifa, Mwenyekiti wa CCM Rais Samia, Makamu Mwenyekiti Stephen Wasira, Katibu Mkuu Balozi Dk. John Nchimbi au MNEC yeyote, kwamba amemtuma akatie Nia ya kupataa ridhaa hiyo kwa ahadi ya kuwabeba au kuwa migongoni mwao”.alisisitiza Ndele.
Ndele amewakumbusha wana Mbeya kwamba, yeye bado anaendelea kuwa Mdau wa Maendeleo wa kuwasaidia Watoto wanaokatisha elimu, kuwapatia mitaji akina mama lishe ili wajitegemee, na sasa ana Mpango wa kuwaunganisha Wajane ambao wamesahaulika ili kuwainua kiuchumi na kijamii, na si kupenda vyeo.
Aidha MNEC Ndele, amewatakia heri watia nia wote (wa Udiwanini na Ubunge), na kuwashauri kwamba, kwa sasa hivi si wagombea bali ni watia nia! Watakuwa qagombea mara tu baada ya michakato ya uteuzi wa watia nia, na kupatikana Watu watatu watakaoridhiwa na CCM, ambao watapelekwa kwa wananchi ili nao watoe baraka zao.
Hata hivyo, Ndele hakuacha kuwashukuru Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya kwa Umueledi wa kuwahabarisha wananchi kwa wakati, ambapo amewaomba wakitaka habari sahihi wasizipokee mitaani, bali wawasiliane na watendaji wa CCM Kata, Wakurugenzi, ambapo wasipokuwa na taarifa, wataziomba kwenye ngazi husika. Mkishndwa kabisa basi mtazipata kwa Katibu Mkuu wa Chama Balozi Nchimbi.
Jibu hilo lilifuatia swali lililoulizwa na mmoja wa waandishi kwamba, waende na jambo gani, maana pia kuna fununu za kwamba, upo ukabila katika mchakato wa watia nia anaowabeba, ambapo alikanusha vikali kuhusu uchafuzi huo akiwataka kupata Habari kwenye vyanzo sahihi ili kudumisha umoja!
