Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihudhuria Sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Comoro leo tarehe 06 Julai, 2025. Mhe. Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizo.