Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 08, 2025 anafungua kikao kazi cha Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (IACC).
Kikao hicho kinatoa nafasi kwa viongozi na watumishi wa TRA kufanya tathmini ya kazi, kuona wapi imefanya vizuri, wapi kuna mapungufu na kujiwekea mikakati ya kuimarisha utendaji katika mwaka mpya wa fedha.



