Ratiba ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 imetoka ambapo kuanzia tarehe 09-27 Agosti itakuwa ni zoezi la kuchukua fomu za uteuzi kugombea kiti cha Urais na Makamu wa Rais.

Tarehe 14-27 Agosti zitakuwa ni tarehe za kuchukua fomu za uteuzi kugombea kiti cha ubunge na udiwani huku tarehe 27 Agosti saa 10:00 Jioni ikiwa ni siku ya uteuzi wa wagombea wa kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani.

Tarehe 28 Agosti hadi tarehe 28 Oktoba itakuwa ni kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Bara huku tarehe 28 Agosti hadi 27 Oktoba ikiwa ni kipindi cha kampeni kwa Zanzibar ili kupisha kura ya mapema Zanzibar itakayopigwa Oktoba 28.

Tarehe 29 Oktoba ndio itakuwa siku ya kupiga kura nchini Tanzania.