Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kisarawe
Chama ACT -Wazalendo kimesema kuwa kimepokea taarifa ya uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi katika ngazi ya majimbo na kimeanza uchunguzi wa kujiridhisha kama wasimamizi hao si makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 7, 2025 na Naibu Katibu Habari, Uenezi na Mahusiano wa Umma Ado Shaibu ametoa kauli hiyo akiwa kwenye mkutano mkuu wa Jimbo la Kisarawe uliofanyika mjini Kisarawe, ambapo alikuwa ni mgeni rasmi katika mkutano huo.
Amesema uchunguzi wa awali wa ACT Wazalendo umebaini kuwa hoja ya kuwaondoa Wakurugenzi wa Halmashauri imezingatiwa kwenye majimbo mengi, na kwamba jambo hilo linakaribishwa kwa mikono miwili.
Hata hivyo Ado amesema chama kimeanza uchunguzi wa kina kujiridhisha kuwa hakuna makada wa Chama cha Mapinduzi, katika orodha ya wasimamizi waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi.
