Na Crecensia Kapinga, JamhuriMedia, Ruvuma
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumjeruhi mke wake (majina yamehifadhiwa) kwa kumchoma na kisu tumboni upande wa kushoto hadi utumbo kutoka nje baada ya kugundua kuwa mkewe alikuwa akitumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV) kwa kificho
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Marco Chilya amesema kuwa mtuhumiwa baada ya tukio hilo aliamua kuchukua sumu ya kuulia wadudu kwenye mashamba ya kahawa (Kimatila)na kuinywa kwa lengo la kutaka kujiua.
Kamanda amesema kuwa mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo mara baada ya kugundua kuwa mwanamke wake amekuwa akitumia ARV kwa kificho hivyo akiamijinkuwa na yeye tayari ni muathirika kitendo ambacho kilisababisha hasira na kuchukua maamuzi hayo.
Kamanda amesema majeruhi amelezwa katika kituo cha Afya cha Tingi akiendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri .
Pia mtuhumiwa amekamatwa na yuko chini ya ulinzi mkali wa Polisi huku nae akiendelea kupatiwa matibabu na mara baada ya afya yake kuimarika atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.



