*Ni kwenye dua aliyowaalika Dk Chakou Tindwa na Abdalla Ulega.
*Asema jimbo linataka mtu muungwana kwa wananchi
*Asisitiza wachague mtu asiyewafunga funga
*Wananchi waunga Mkono,wazungumza
Na Mwandishi Wetu JamhuriMedia, Mkuranga
Mbunge wa zamani wa jImbo la Mkuranga, Adam Kigoma Malima,amewataka wakazi wa jimbo hilo,kutokurudia makosa waliyoyafanya miaka mitano iliyopita ya kuchagua kiongozi, asiyejihusisha na shida za wananchi zaidi ya kuwashughulikia wakososaji wake kwa kuwafikisha katika vituo mbali mbali vya Polisi kama sehemu ya kuzuia sauti zao.
Malima ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,alitoa kauli hiyo juzi katika wilaya ya Mkuranga wakati akifanya dua ya kuwarehemu, wazee wa mji wa Mkuranga waliotangulia mbele ya haki, ambapo aliwaalika watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani wa jimbo hilo.
Alisema wana Mkuranga wanapaswa kumchagua mtu muadilifu,asiyetumia nafasi yake ya madaraka kuwanyanyasa wengine kwa kuwa maadaraka yanampata mtu na kuondoka ilihali mahusiano ya kindugu yakibaki wakati wote.
Katika dua hiyo ambayo Malima aliwaalika watia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Mkuranga Dk Chakou Khalfan Tindwa na Abdallah Ulega ni Tindwa pekee aliyehudhuria huku Malima akitaja kuwa mwingine, amegoma kuhudhuria hafla hiyo.
“Hatuwezi kufikia ubora wa Mwenyezi Mungu, lakini huyo mtu tutakayempa uongozi ni lazima awe rahimu,awe na mapenzi na ninyi asiwe na tabia ya kuwafunga funga wenzake kila wanapomuuzi nyie mlikuwa mnaniudhi tena kuna wengine walikuwa wananitukana halafu wanakuja kuniomba nauli tena wakati huo mimi Waziri lakini sijamuita Polisi kumwambia chukua hawa waweke ndani”alisema Malima na kuongeza.
“Bahati mbaya sana yule mdogo wangu na huyu mdogo wangu,wote wadogo zangu huyu maana yake huyu aliyeingia nimewakaaribisha wote yule kagoma kuja, huyu kaja nami si Simba wala Yanga,ila huyu aliyekuja anafanana kidogo tabia na mimi yule mwingien Hapana”alisema Malima.
Akielezea sababu ya kutochukua fomu ya Ubunge Malima alisema,jukumu lililopo ni kuhakikisha wanamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan,katika maeneo waliyokabidhiwa na kwamba hanaa shaka na nafasi ya Rais Samia katika jimbo hilo kwa kuwa wananchi wanamuelewa.
Wakizungumzia kauli hiyo ya Malima baadhi ya wananchi waliohudhuria dua hiyo,walieleza kuwa alichoeleza kina uhalisia ndani ya jimbo hilo huku wakitolea mfano wa baadhi ya watu walioenda tofauti na Mbunge aliyemaliza muda wake walivyoshughulikiwa.
“Mkuranga inahitaji mtu muungwana,mimi nakumbuka kuna diwani mmoja,alishawahi kusema shida yao kubwa ni maendeleo na alimwambia mbunge wake wakati huo,atomize wajibu wake,lakini badala ya kumsikiliza akaendaa kushughulikiwa kwenye vikao vya chama,wengine mpaka tuliitwa kuhojiwa Takukuru nah ii yote ni nguvu ya aliyekuwa Mbunge wetu”alisema Salim Jumaa.
Mkazi mwingine wa Kiparang’anda aliyejitambulisha kwa jina la Sudi Kanoga,alisema miaka mitano iliyopita walikuwa na mbunge aliyekuwa akijitaamba kuwashughulikia wenzie kwa gharama yeyote.
Kanoga alisema miongoni mwa watu waliokutana na ghadhabu hiyo ni pamoja na Juma Abeid na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Sudi kuwa walikuwa miongoni mwa watu waliobambikwa kesi.
