Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-WazeldnoTaifa, Ado Shaib, ameongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Taifa cha chama hicho kilicholenga kupitia masuala mbalimbali ya kiutendaji, yakiwemo maandalizi ya kikao kijacho cha Kamati Kuu.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama, zilizopo Vuga, Mjini Unguja, na kilianza rasmi saa nne kamili asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, mkutano huo ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha Kamati Kuu ya ACT-Walendo, kinachotarajiwa kufanyika katika Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, mnamo tarehe 17 Januari 2026.
Kikao cha Kamati Kuu kinatarajiwa kujadili masuala muhimu ya mwelekeo wa chama, tathmini ya shughuli za kisiasa na mikakati ya kuimarisha uendeshaji wa chama kitaifa.











