Katika mwendelezo wa programu ya kukutana na makundi mbalimbali kwenye jamii, jana tarehe 25 Oktoba 2025, mgombea wa Ubunge Jimbo la Tunduru Kaskazini Ndugu Ado Shaibu Ado amekutana na kufanya mazungumzo na Mama Lishe wa Tunduru Kaskazini kwa ajili ya kuwaomba kura. Kikao hicho kilihudhuriwa na mafundi wa ushonaji.

Ndugu Ado ametumia tukio hilo kusikiliza changamoto za makundi hayo na kuwaomba kura zao.

Wakitoa changamoto zao, Mama Lishe wa Tunduru wamesema changamoto sugu za Tunduru ni ukosefu wa mitaji, gharama za juu za kupangisha vibanda na kukithiri kwa rushwa kwenye mikopo ya serikali kwa wajasiriamali.