Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo, amefariki dunia leo tarehe 19 Februari 2026 majira ya saa 4:00 usiku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Kardinali Pengo amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

“Ninayo masikitiko makubwa kuwatangazieni kwamba leo tarehe 19/02/2026 saa 04:00 usıku huu mpendwa baba yetu Mwadhama Polyearp Cardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaatu wa Jımbo Kuu la Dar es Salaam, ameitwa nyumbani kwa Baba wa Milele akiwa katıka Tasısı ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Taarifa za mazishi zitawajia mara baada ya mipango kukamilika. Tumwombee apumzike kwa amani.

Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa
Amani; Amina.”

Taarifa hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Thaddeus Ruwaichi