Ryan Routh amepatikana na hatia ya kujaribu kumuua Rais Donald Trump kwenye uwanja wa gofu wa Florida Septemba mwaka jana.
Mahakama ilimpata Routh, 59, na hatia ya mashtaka yote, ikiwa ni pamoja na jaribio la mauaji ya mgombea mkuu wa urais na makosa kadhaa ya kutumia silaha.
Tukio hilo lilitokea tarehe 15 Septemba 2024 wakati Trump, ambaye wakati huo alikuwa mgombea urais, alikuwa akicheza gofu kwenye uwanja anaoumilik uliopo katikaufukwe wa West Palm Beach, takriban dakika 15 kutoka kwa makazi yake ya Mar-a-Lago.
Routh alijaribu kujidhuru baada ya hukumu kusomwa, kulingana na mshirika wa BBC wa Marekani, CBS News. Inasemekana alijaribu kujichoma kisu kwa kutumia kalamu kabla ya Wanajeshi wa Marekani kuingilia kati.
Katika chapisho la mtandao wa kijamii mara baada ya hukumu hiyo, Trump alishukuru vyombo vya sheria na shahidi ambaye alitoa taarifa zilizofanikisha kukamatwa kwa Routh.
Trump alisema kuhusu Routh: “Huyu alikuwa mtu muovu mwenye nia mbaya, na walimkamata. Wakati mkubwa sana kwa HAKI NCHINI AMERIKA!”.
Mwanasheria mkuu wa serikali Pamela Bondi alisema: “Jaribio hili la kumuua halikuwa tu shambulio kwa rais wetu, bali ni dharau kwa taifa letu.”
