Katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Mei 8, 2025 limefunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi namba 11041/2025 mbele ya Onesmo Nicodemo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Simanjiro Samuel Warioba Gunzar.

Mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa ya ufujaji na ubadhirifu Kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 R. E 2022, ikosomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza kifungu cha 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na pamoja na Makosa ya Kupangwa Sura ya 200 R:E 2022, na kosa la wizi akiwa mtumishi wa umma kinyume na vifungu 258, 265 na 270 vya Kanuni za adhabu (sura ya 16 R.E 2022).

Akisoma hati ya mashtaka Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Faustin Mushi amesema mshtakiwa wakati akitekeleza majukumu yake kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Simanjiro alitumia fedha za Halmashauri kiasi cha shs. 5,000,000 kwa matumizi yake binafsi.

Mshtakiwa amekana kutenda makosa yote yanayomkabili na shauri liliahirishwa hadi 27/05/2025 kwa ajili ya kusikilizwa hoja za awali (PH).

Kwa sasa mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana kwa kuea ametimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya sh. 7,000,000/-