Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema kuwa baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi wamekuwa wakidai kuwa msaada wa Rais, Dkt. Samia ni sehemu ya hongo, madai ambayo yamekuwa yakimuumiza sana kama kiongozi wa dini. Niendelee kumsihi Rais Samia asirudishwe nyuma na watu hao bali aendelee kuwa na hofu ya Mungu katika kusaidia huduma za kiroho nchini.
Askofu Mkuu Shoo amebainisha hayo Julai 03, 2025 Jijini Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Kikristo nchini Tanzania – CCT ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo.

