Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amefungua mafunzo ya viongozi wa majimbo ya Kanda ya Kati mjini Dodoma.

Akifungua mafunzo hayo Aprili 12, 2025 jijini humo, Ado amewaeleza viongozi wa majimbo yote 25 ya mikoa ya Dodoma, Manyara na Singida kwa niaba ya viongozi wa taifa ni kwa nini chama hicho kimesaini Maadili ya Uchaguzi.

Ado amesema chama hicho kinaongozwa na shabaha ya chama ambayo ni kuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika kuleta maendeleo ya watu.

Amesema shabaha hiyo haiwezi kutimia bila chama kushiriki na kushinda chaguzi ili kuunda serikali na kutekeleza sera zao.