Tangu vita vilipoanza, bei ya pipa moja la mafuta ghafi imepanda kutoka dola 73 hadi takribani dola 117 kwa sasa.
Kwa kawaida, kupanda kwa bei ya jumla ya nishati huonekana kwanza kwenye vituo vya mafuta, na hali hii inaonekana kote duniani.
Nchini Marekani, wastani wa bei ya petroli umeongezeka kwa zaidi ya dola moja tangu kuanza kwa mgogoro huo, na kufikia zaidi ya dola 4 kwa mara ya kwanza katika karibu miaka minne.
Nchini Uingereza, wastani wa bei ya petroli umeongezeka kwa asilimia 14, na dizeli kwa asilimia 27.
Baadhi ya nchi, kama Sri Lanka na Bangladesh, zimeanza kuweka mgao wa mafuta, na wiki iliyopita Slovenia ilikuwa nchi ya kwanza katika Umoja wa Ulaya kufanya hivyo.
Nchini Australia, kodi ya mafuta imepunguzwa kwa nusu kwa muda wa miezi mitatu ili kusaidia madereva kukabiliana na bei kubwa za mafuta, huku majimbo mawili yakitoa usafiri wa umma bure kwa muda ili kuwahamasisha watu wasitumie magari yao.

