Na Ruja Masewa, JamhuriMedia,Rungwe
Baada ya kuchangia maendeleo mara nyingi ikiwemo Ujenzi wa Madaraja katikaJimbo la Rungwe mkoani Mbeya, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwaiteleke Foundation Aliko Anyambilile Mwaiteleke, sasa anautaka ubunge Rungwe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aliko aliyejitolea kutunza watoto wa shabiki wa Simba aliyefariki kwa ajali gari alisema hayo Juni 7, 2025 alipozungumza na Vyombo vya Habari, familia, ndugu, Marafiki na Wananchi, akitangaza rasmi nia yake ya kugombea Ubunge, mara tu chama chake kitakapotoa fomu.

Akizungumza katika Wito huo Aliko alidai, baada ya kushirikiana nao katika shughuli nyingi za Maendeleo jimboni humo, na ushawishi alioupata miongoni mwao, CCM kitakapotoa fomu, naye ataomba kuwa kwenye kinyang’anyilo cha kuwania Ubunge wa Rungwe.
Katika Wito huo Aliko alisema, Juni 29-30, 2025 mjini Dodoma Chama chake na Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu walitangaza nafasi za uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.
” Ndugu Wananchi. Mimi Mtoto wenu na Kada wa CCM; Nmewaita ninyi na Wanahabari, ili kuwajulisha; Natangaza rasmi nitakuwa mmoja wa watakaoomba ridhaa ya Utumishi wa Jimbo hili (Rungwe)”.alisema na kushangiliwa.
Akijibu swali la mwandishi Moses Aswile wa Rungwe FM na Tukuyu Online TV, Aliko alisema umri mdogo si sababu, anao uwezo wa kusimamia mambo, na ni mzaliwa na mkazi wa jimbo hilo anayefahamu changamoto zake zote. “Nia ninayo; Uwezo ninao tusubiri muda ufike”.

Hata hivyo wakati watie nia wengi nchini, hivi sasa ni kama mabikira
wanaojipaka mafuta ya manemane, kujipaka manukato na vipodozi mithiri ya washindani wa shushani ngomeni kwa mfalme wakisaka umalkia, Aliko alikataa kusema chochote, mipango au vipaumbele vyake hadi muda ufike!.
Kati ya tarehe 28 Juni -2 Julai 2, 2025, CCM kinatarajia kutoa fomu za kuomba kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge ambapo watia nia mbalimbali watajitosa kuchuana ili kusaka nafasi za kukubaliwa kuwawakilisha wananchi.

