Bakari Kimwanga ambaye alikuwa anatetea nafasi yake ya udiwani kata ya Makurumla Mkoa wa Dar ea Salaam amefanikiwa kurejea tena kwa kupata kura 467 ambapo Rajab Suleiman Hassan alipata kura 344 na Idd Shaban Taletale ameambulia kura 18.

Kati ya madiwani 19 katika Halmashauri ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam ni madiwani watatu tu ndio waliofanikiwa kutetea nafasi zao.