Na Jumbe Ismailly, JamhuriMedia, Singida
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida limewaagiza masheikhe wa wilaya pamoja na maimamu wa misikiti wote Mkoani hapa kutoviruhusu vikundi vya Wahadhiri na Wanaharakati kutumia majengo ya ibada kupotosha waumini wao kwamba suala la kupiga kura ni haramu.
Sheikhe wa Mkoa wa Singida, Alhaji Issah Nassoro Issah ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumzia tabia iliyoanza kujitokeza hivi karibuni ya baadhi ya Wahadhiri na Wanaharakati kutumia majengo ya ibada kupotosha waumin iwa dini ya Kiislamu kwa kuwahamasisha kwamba suala la kupiga kura ni haramu kwa mujibu wa maandiko ya dini hiyo.
Alhaji Issah ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo Mkoa wa Singida aliweka bayana kwamba katika siku za hivi karibuni kumeanza kujitokeza vikundi vya, Wahadhiri na Wanaharakati wanaopita kwenye baadhi ya mikoa, wilaya, kata pamoja na misikiti kuhamasisha kwamba suala zima la uchaguzi kuwa ni haramu na kwamba jambo hilo katika uislamu halipo.

“Mimi kama sheikhe wa Mkoa wa Singida na kama msemaji wa Mkoa na ni mwakilishi wa Mheshimiwa Mufti katika Mkoa wa Singida, nasema kwamba watu hao hatuwataki ndani ya Mkoa wetu wa Singida na natoa oda kwa waislamu na waumini, maimamu, masheikhe wa Kata, masheikhe wa wilaya katika wilaya zenu wasiruhusiwe kupokelewa na kuingia katika misikiti yetu na kuanza kuhadhiri na kuanza kuelekeza kwamba suala la uchaguzi kwamba ni haramu” alisisitiza sheikhe huyo wa Mkoa wa Singida.
Akizungumzia kuhusu sula la kwamba mwanamke kutoruhusiwa kuwa kiongozi kwamba uislamu unapinga mwanamke kuwa kiongozi kuna baadhi yao wamekwenda mbali zaidi na kusema iwapo kama mwanamke anaruhusiwa kuwakiongozi basi aruhusiwe pia kuwa imamu wa msikiti ili aweze kusalisha, dhana ambayo kiongozi huyo amepingana nalo na kisha kutoa ufafanuzi wa kidini unavyoagiza.
Kwa mujibu wa sheikhe huyo wa Mkoa kuna masuala mengi yanayofanyika nje ya kuwa na kiongozi mwanamke ambayo ni mengi kama vile kuna nguruwe, kuna mabucha ya nguruwe, kuna nyama za nguruwe ambayo hayo nayo hayatakikani hivyo basi kwa matakwa ya wahadhiri hao hata nguruwe basi hayatakiwi kuwepo na mabaa hayatakiwi kuwepo.
“Lakini nchi yetu haina dini ni nchi ambayo inakuwa inajiendesha kwa sekula na katiba maalumu na katiba yake siyo ya biblia wala katiba yake siyo ya korani, kwa hiyo kama katiba tunayoifuata ya kuchagua kiongozi wa nchi hii basi hatuifuati katiba ya biblia wala hatuifuati katiba ya korani bali tunafuata katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania