Na Mwandishi Wetu

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaririki Mhe. Balozi Shaib Mussa amempokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyrus Mhe. Constantinos Kombos, katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Mhe Mussa aliambatama na Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika Mhe. Balozi Swahiba Mndeme na Maafisa Wandamizi wa Wizara.

Kwa upande wake Mhe. Kombos ameambatana na ujumbe wa watu sita kutoka katika Wizara yake, Mabalozi na wawakilishi kutoka Idara Siasa na Afrika.

Ziara ya Mhe. Kombos ya tarehe 8-10 Julai, 2025 inalenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kikanda na Tanzania, ili kuleta maendeleo ya wananchi wa pande hizo mbili.

Akiwa nchini, Mhe. Kombos atakutana Viongozi wa Kitaifa, na kufanya mazungumzo na Mhe. Waziri-NJE Mhe Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Aidha, atashiriki mkutano wa pande mbili kati ya Tanzania na Cyprus, atatia saini hati za makubaliano ya ushirikiano kuhusu Mashauriano ya Kisiasa na ile ya ushirikiano katika masuala ya Mabaharia.

Mhe. Kombos pia atashiriki katika majadiliano ya meza ya pamoja kati ya Jumuiya ya Biashara ya Ulaya na Tanzania Chambers of Commerce.