Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Viwanda vya Nyama na Uvuvi kutoka Uganda, Kyakulaga Fred Bwino pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Fred Mwesigye, leo Mei 27 jijini Dodoma.
Katika Mazungumzo hayo wamejadiliana kwa kina kuweka makubaliano ya kimaandishi kushirikiana katika kukuza sekta kilimo hususani upatikanaji wa mbolea na pembejeo za kilimo, kuona uwezekano wa kampuni ya Itracom Fertilizer ya jijini Dodoma kuuza mbolea yake nchini Uganda.
Aidha, wamekubaliana kuimarisha mifumo ya usafirishaji wa bidhaa za Kilimo pamoja na kubadilishana uzoefu katika kilimo cha kahawa.


