Na Mwandishi Wetu JamhuriMedia, Tabora

Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amewataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kutunza vema historia ya
Chama hicho.


Amesema mkoa huo una historia ya kipekeee kwani mwaka 1958 chama hicho kulifanya mkutano maalumu ulikuwa na lengo la kujenga na kukiimarisha kwa manufaa ya Watanzania wote.


Amesema mkutano ndiyo msingi ambao umesaidia CCM kuendelea kuwa imara mpaka sasa.


Amesema kutokana na hali hiyo wagombea wote wa ubunge na udiwani wanapaswa kutumia busara za wazee waliopo Stephen Mashishanga na Nassoro.Hamdani.


Amewataka Watanzania waendelee kuwa na Imani na CCM pamoja na mgombea urais, Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri aliyofanya.


“Tukizungumza vijana mana jambo lenu, kina baba na kina mama, hata wazee nao wana jambo lao, nanyi wagombea wa CCM fuateni nyayo za mgombea urais wetu mkawasikilize waze,”amesema.


Mgombea ubunge wa Jimbo la Urambo ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wa mkoa huo, Magreth Sitta ameelezwa kuwa na ushawishi mkubwa wa kusuluhisha migogoro.


“Mama Sitta ndiye kiongozi wa wabunge akiingia ofisini kwako haondoki bila kupata anachokitaka,”amesema.