BEI ya mafuta imepanda leo Jumatatu huku masoko ya hisa yakiropomoka kutokana na kishindo cha mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yaliyoanza siku ya Jumamosi.
Pipa moja la mafuta ghafi limefikia karibu dola 80 kwenye soko la dunia ikiwa ni ongezeko la wastani wa asilimia 7.5 ya bei ya wiki iliyopita.
Wasiwasi ni mkubwa kwamba bei ya nishati hiyo huenda itapanda zaidi mnamo siku zijazo katika wakati hakuna dalili kwa mzozo wa kijeshi wa Mashariki ya Kati kutulia.
Rais Donald Trump wa Marekani ameashiria jana Jumapili kuwa mashambulizi ya nchi yake pamoja na Israel nchini Iran yanaweza kuendelea kwa hadi wiki nne zijazo.


