Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Kampuni kinara na mvumbuzi wa kimataifa katika tasnia ya michezo ya kubashiri mtandaoni imezindua rasmi mashindano ya kwanza ya Aviator Legends.
Taarifa iliyotolewa Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa shindano hili la kusisimua linawakaribisha watu wote kujaribu ujuzi, ujasiri na muda sahihi katika kurusha Kindege cha Aviator.
Mashindano ya Aviator Legends yanatarajiwa kuwa tukio kubwa zaidi la mchezo wa “Crash”kwa mwaka huu, kukiwa na fursa kwa wachezaji kokote Tanzania kushindania zawadi kubwa, Miruko ya bure kila siku na nafasi ya kipekee kutangazwa kuwa Aviator Legend wa mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashindano hayo yalianza Juni 2, 2025 hadi Juni 30, 2025 ikihusisha washiriki waliojisajili na Betway kupitia www.betway.co.tz na kusisitiza kuwa jukwaa ni Betway peke yake.
“Zawadi kuu ya Tsh. 57,500,000 itatolewa kwa mshindi na miruko ya bure kila siku,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa washiriki wanapaswa kucheza Avitaor kwa dau la kuanzia Tsh. 400 kwa kipindi chote cha mwezi wa sita. Rusha Kindege Mara nyingi kisha Cashout ili kujikusanyia Pointi za ushindi.
Kwa mujibu wa aarifa hiyo, kadri Kindege kinavyoruka kwa muda mrefu ndio pointi zako za ushindi zinavyoongezeka zaidi ila ukichelewa kucashout unakuwa umepoteza.
Pointi zako zitahesabika kuzingatia viwango vya multiplier na uthibiti wa mchezaji. Washiriki 8 wa juu kwenye orodha ya vinara mwishoni mwa shindano wataingia kwenye fainali kubwa zaidi itakayofanyika Dar es salaam ambapo watapata nafasi ya kushinda zawadi kubwa zaidi ya Tsh. 57,500,000 na kutangazwa kuwa Aviator legend wa 2025.
Calvin Mhina, Meneja Masoko wa Betway alisema, “Tunataka kuleta uzoefu wa kipekee kwa kuzindua shindano litakalowahamaisisha wachezaji kuchukua nafasi ya kushinda na kukuza ushindani mzuri kati yao.
Mchezo wa Aviator uliotegenezwa na SPRIBE umekuwa maarufu sana nchini Tanzania kutokana na kasi, kueleweka kirahisi na uwezekano mkubwa wa ushindi.
Giorgi Tsutskiridze – Afisa Mkuu wa Biashara wa SPRIBE aliongeza, “Aviator imebadilisha dhana ya michezo ya Crash, unaeleweka kirahisi na unavutia zaidi. Ushirikiano wetu na Betway katika kuzindua mashindano ya kwanza kabisa ya Aviator Legends ni hatua ya kufikisha burudani hii kwa watu wengi zaidi. Shindano hili si la zawadi tu, ni kuhusu kujenga jumuiya ya wachezaji wanaothubutu kuvuka mipaka na kufuata safari bora zaidi. Tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio haya.”
Aliendelea kusema kuwa Kwa kutumia jukwaa thabiti na linaloaminika zaidi la Betway mashindano ya Aviator Legends yanahakikisha kutoa uzoefu wa kipekee kwa wachezaji wa muda mrefu na wapya pia.
“Kwa zawadi kubwa za pesa na nafasi ya kuwa Aviator Legend, Betway inawahamasisha wachezaji kurusha kindege cha Aviator na kujiunga na Malegend kwa kujisajili au kuingia. Haijalishi kama wewe ni mchezaji wa kawaida au mwenye kuweka madau makubwa, hii ni nafasi yako kuchana anga na kuibuka Mshindi,” alisema.
