Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media- Bukombe
Mgombea ubunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita na Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko amesema mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amefanikisha ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya baada ya kupita miaka 29.
Biteko ametoa kauli hiyo alipopewa nafasi ya kuhutubia maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia leo Oktoba 12.
Kama mtenda mujuuza toka wilaya ya Bukombe imeanzishwa mwaka 1996 hatukuwa na jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ilikuwa ni ofisi ya tarafa wakati tukiwa wilaya ya Kahama, mama umesema piga chini jenga tunanyanyua ghorofa kwa ajili ya jengo la utawala, hatukuwa na soko la kisasa,ukienda pale utakuta mabati yamezungushwa Wachina wanapishana wanajenga kwa ajili ya watu wa Bukombe.
Hatukuwa na stendi ya maana, iliyokuwapo ilikuwa ikishenyesha mvua watu wanaingia kwenye mabasi wamekunja suruali zao kwa sababu ya kujaa maji kama majarubani, shilingi bilioni 25 ziko pale tuseme nini.Umetukuta tuna mtandao wa barabara kilometa 256 kama muujiza, hivi sasa mtandao wetu kilomita 1,400 ukitaka kwenda kona yoyote huhitaji nyingi uliingilia,amesema.

Amesema barabara ya kutoka Ushirombo kwenda Katoro wananchi walikuwa wanateseka kila siku wanalia vumbi jingi.
Wananchi walikuwa wanalia wanasema mwambia mama atusaidie, nilivyokufuata ukaniambia hili jambo haliko kwenye Ilani, kwa sababu ya mipango hatujajipanga nipe muda, nilijua imeishia hapo, lakini tena kwa hali ya ajabu hukunipa taarifa na mrejesho nikashangaa naambiwa sasa tunatangaza barabara ya kwenda kwenda Ushirombo-Katoro lami, kule mitaani tulikuwa hatujui lami kote umetandika, umetuwekea na taa watu wafanyabishara mpaka usiku.
Kama haitoshi ulijua kama bingwa wa mipango ya maendeleo, ukasema leo nataka watu wa Bukombe wawe bize, mahali watu wakiwa hawako bize watakuwa na majungu, wewe hukutaka majungu watu wafanye kazi, ukaniuliza ni jambo gani likifanyika Bukombe itakuwa bize, nilikuja kwako kwa kuoga maana tulijaribu huko tukaogopa.
Nikakuomba mama watu wetu wangechimba dhahabu changamoto kubwa iliyopo hawaruhusiwi kuingia kwenye yale maeneo, ukaniambia ngoja tuangalie sheria najua itachukua muda.nataka niwe shuhuda mbele yako na mbele ya mwenyezi Mungu, wewe kitendo cha kuruhusu watu hawa wakachimbe kule tena kwa utaratibu ukawapa na leseni zidi 7,000, leo mji wa Ushirombo ukifika hapa mgeni unakosa pakulala kwa sababu pote kumejaa watu wanashughulika hakuna kijiwe ukute watu wamekaa kila mmoja yuko bize,amesema.
Amesema Rais Samia alitambua watu wakiwa hawana fedha mfukoni wanaanza kuwa na majungu, jambo ambalo limeondolewa kabisa katika eneo hilo.
leo mama watu wa hapa wanaongea Kiswahili wananchanganya na Kiingereza ukiwajuliza wanasema wanajibu any way give me time, nasimama mbele yako utembee kifua mbele mambo mengi unayotufanyia hukuwahi kuyaahidi hayoko kwenye Ilani, lakini umetutendea maajabu.
Pale Kilimahewa tunajenga uwanja wa mpira wa kisasa, tena Azam wamekubali kutufungia taa, uwanja ule utakuwa michezo ya mchana na usiku, hukuishia hapo eneo lote la uwanja umezungusha lami kila kona kutawekwa taa.

Nakushukuru sana, nakushukuru kwa heshima ulionipa utu ndiyo kitu pekee ambacho mtu atakumbukwa nacho nitaendelea kujifunza kwako, nitaendelea kuwa mnyenyekevu na mtiifu kwako na kwa kweli baada ya kunipa kazi ya kuwa msaidizi wako wa karibu nataka kukushukuru tena mbele ya wazazi wangu na wana Bukombe.
Nakuahidi mbele ya watu wa Bukombe nitaendelea kuwa mwanifu, mtiifu mtu ninayekusikiliza sana wakati wote wa maisha yangu kwa sabau umeweka sahihi kubwa kwenye wilaya yetu na kwenye maendeleo, Mungu akubariki , watu hawa walivyojua unakuja huwa wanaona watu wanakwenda kwenye mikutano na vikabu, ndoo, nikawakuta kina mama pale wakaniambia niwanunulie masimu tenki twenda nayo, nikawaambia mkipeleka haya yatakuwa vurugu,amesema.
Amesema wananchi wa wilaya hiyo hawachukulii uchaguzi kirahisi rahisi, bali kama uhusiano wa maisha yao ndiyo maana wamejipanga kumchagua.


