Na Lookman Miraji, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Katika kuelekea msimu wa tatu wa tuzo za michezo ambazo hutolewa kila mwaka kwa kuwathamini wanamichezo waliofanya vizuri kwa mwaka husika baraza la michezo la taifa(BMT) limesema kuwa tuzo hizo zinatarajiwa kuwa na upekee mkubwa tofauti na miaka iliyotangulia.
Akizungumza Mtendaji mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Neema Msitha amebainisha kuwa tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu, huku tuzo hizo zikilenga kuwatambua wanamichezo katika michezo mbalimbali waliofanya vizuri kwa mwaka uliopita.

Aidha tuzo hizo pia zitawatambua watu wa fani mbalimbali za michezo zikiwemo makocha na hata waandishi wa habari za michezo watakaobainika kuwa wamekuwa na mchango wa kipekee katika kuripoti habari za michezo nchini.
Kwa upande mwingine pia, BMT limeendelea kuviasa vyama vya michezo nchini kuendelea kuzingatia kalenda na mipango iliyojiwekea kwa mwaka huu 2025.
