JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Sitanii

Tusiibeze bajeti, tusiishangilie

Juni 9, mwaka huu, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, aliwasilisha bajeti ya Serikali bungeni kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Bajeti hii imeficha siri nzito yenye mwelekeo wa kuliondoa Taifa letu katika aibu ya kuwa ombaomba. Ni kweli,…

Rais Magufuli wekeza upate kodi

Wiki iliyopita niliandika makala juu ya kijana aliyefuga kuku huko Singida. Nimebaini kuwa ufugaji ule umekuwa kivutio kikubwa kwa wengi waliosoma makala yangu. Hata hivyo, ingawa wengi walitaka kuwasiliana naye awafundishe, kijana huyo anasema yeye alifundishwa na mwalimu kutoka Chuo…

Rais Magufuli epuka ushauri huu!

Wiki iliyopita nilikuwa katika kipindi cha ‘Malumbano ya Hoja’ kinachorushwa ‘live’ na ITV. Mjadala kadiri ulivyoendelea nilipata shida kidogo. Niliwaona baadhi ya wachangiaji wakizungumza lugha ya hatari, ambayo ninaisoma katika baadhi ya magazeti. Wanasema Rais John Magufuli anahujumiwa.  Sitanii, neno…

Hongera Magufuli, ila sukari, matrafiki…

Wiki iliyopita nilipata fursa ya kuzungumza na mtu mmoja mzito. Mazungumzo yetu yalikuwa ni kwa maslahi ya Taifa. Tulizungumzia ustawi wa Taifa letu na mwelekeo wa nchi chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli. Mazungumzo yetu yalijaa nia njema,…

Dk. Mwakyembe anaiaibisha PhD

Wiki iliyopita nilikuwa bungeni hapa mjini Dodoma. Niliingia katika ukumbi wa Bunge, nilisikiliza michango ya wabunge kadhaa. Nilimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, na wengine wengi. Niseme mapema tu kuwa hapa leo najadili hoja ya Bunge…

Nani anamtuma Dk. Tulia?

Katika siku za karibuni imekuwapo mitafaruku kadhaa bungeni. Tumesikia habari za Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwa na mikwaruzano na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson. Nakumbuka Dk. Tulia alivyokuwa mbunge wa kwanza kuteuliwa katika vile viti 10 vya…