Bandari Bagamoyo, kifo cha Bandari Dar
Imenichukua miaka miwili kufikiri juu ya hiki kinachoitwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Ujenzi huu ulianza kutajwa mwaka 2010, na ilipofika Machi 2013, Rais wa China, Xi Jinping, akatia saini mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo. Mkataba ukasema bayana kuwa ujenzi huu utatengewa dola bilioni 10. Nilisubiri kusikia Watanzania wanasema nini, ila muda wote naona…