Kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya Kigoma mbele ya Mhe. Anna Kuhungu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kigoma.
Awali wakisoma Mashtaka ya kesi hiyo Na. ECC.9258/2026 dhidi ya washitakiwa Kulwa Ryoba James, Gaudens John Ndolo na Pamhilius Gerald Gagwa
Waendesha Mashtaka kutoka TAKUKURU Bw. Augustino Lohay na James Nyarobi waliieleza mahakama kuwa Washtakiwa wanakabiliwa na makosa ya Matumizi ya Nyaraka Kumdanganya Mwajiri, Ufujaji na Ubadhilifu, Kusaidia kutendeka kwa Kosa na Kughushi; Kinyume na Kifungu cha 22, 28(1) na 30 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 R. E 2022 vikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza na vifungu vya 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Sura ya 200 Marejeo ya Mwaka 2022 pamoja na Kifungu cha 333, 335(a), 335(b)(i)(ii) cha Kanuni za Adhabu Sura 16 Marejeo ya mwaka 2022.
Washtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Julai hadi Agosti 2022 kwa kupitia hati za malipo zenye thamani ya TShs 103,000,000/- mali ya Bodi ya Maji Blonde la Ziwa Tanganyika Kigoma Mjini (LTBWB) ambayo ilkuwa na maelezo ya uongo ya kuwalipa watumishi hewa wakati wa Kutambua na Kukagua vyanzo vya maji katika Wilaya za Kibondo,Kakonko ,Biharamulo na Ngara.
Washtakiwa wamekana makosa yote.
Aidha, Washtakiwa wamepelekwa mahabusu baada ya kutotimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na Mahakama.
Shauri hilo limepangwa kuendelea tena tarehe 14/05/2026

