Chadema la Zitto sawa, hamtambui Mahakama?
Wiki iliyopita ilikuwa ni historia nyingine katika siasa za Tanzania. Tulishuhudia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe akiachia ngazi baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumfukuza uanachama. Zitto amefukuzwa uanachama ukiwa mwendelezo wa harakazi na misigishano ya ndani kwa ndani, kubwa likiwa ni kugombea madaraka. Zilianza kama tetesi, baadae ikathibitika kuwa Zitto…