Category: Kimataifa
Watu 120 wafariki katika ajali ya ndege Korea Kusini
Ndege iliyokuwa imebeba abiria 181 imeanguka katika uwanja wa ndege kusini magharibi mwa Korea Kusini. Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya 09:00 saa za eneo – 00:00 GMT – wakati ilipokuwa ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa…
Jeshi la Kongo ‘ladungua ndege zisizo na rubani’ za Rwanda
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ‘limedungua’ ndege sita zisizo na rubani za Kamikaze za Jeshi la Rwanda katika mji wa Mambasa eneo la Lubero katika Mkoa wa Nord Kivu. Msemaji wa Jeshi Lt Kanali Mak Hazukay alisema waasi…
Waandishi wa habari watano Gaza wauawa
Kituo cha Televisheni cha Palestina kimesema waandishi wa habari watano kutoka kituo hicho wameuawa katika shambulizi la Israeli katika Ukanda wa Gaza katikati. Walikuwa katika gari la Quds Today lililokuwa limeegeshwa nje ya hospitali ya al-Awda, ambapo mke wa mmoja…
Chombo cha anga za juu cha NASA chajaribu kuweka historia kwa kuwa karibu zaidi na jua
Chombo hicho cha Parker Solar Probe kilisafiri katika angahewa ya nje ya nyota yetu, kikistahimili joto na mionzi mikali. Hakitakuwa na mawasiliano yoyote kwa siku kadhaa wakati huu wa joto kali na wanasayansi watakuwa wakisubiri ishara, inayotarajiwa tarehe 27 Desemba,…
Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alazwa hospitalini
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amelazwa hospitalini baada ya kupata homa, kwa mujibu wa msemaji wa chama cha Democrat. “Anasalia katika hali nzuri na anathamini sana utunzaji bora anaopokea,” Angel UreƱa aliandika kwenye X, iliyokuwa Twitter. Alisema Clinton…
Watu 38 wafariki Congo, wengine wapotea
Watu 38 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 100 kupotea baada ya Feri iliyokuwa imejaa watu kupinduka kwenye mto Busira Kaskazini – Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo. Katika ajali hiyo ya Feri ambayo ilibeba watu waliokuwa wakirejea…