Category: Kimataifa
Kenya yaijibu Sudan kuhusu uwepo wa waasi wa RSF jijini Nairobi
Baada ya Sudan kutangaza nia ya kuchukua hatua kali dhidi ya Kenya kwa kile ilichokiita kuunga mkono wanamgambo wa RSF kwa kuwapa nafasi ya kufanya mkutano jijini Nairobi, Kenya imejitokeza kueleza msimamo wake kuhusu suala hilo. Katika taarifa rasmi iliyotolewa…
Jaji aagiza Besigye arejeshwe gerezani
Mwanasiasa maarufu wa Uganda Dk Kizza Besigye amefikishwa katika Mahakama Kuu mjini Kampala kusikiliza ombi la mawakili wake la kumtaka achiliwe huru. Besigye ambaye amesusia chakula tangu wiki iliopita alionekana kudhoofika huku akiandamana na mshtakiwa mwenzake Haji Obeid Lutale. Awali…
Marekani, Urusi zakubaliana kumaliza vita Ukraine
Viogozi wa Marekani na Urusi waliokutana Jumanne mjini Riyadh, Saudia Arabia wamekubaliana kuanzisha mchakato wa amani katika mzozo wa Ukraine licha ya Kiev na washirika wake wa Ulaya kutoalikwa kwenye mazungumzo hayo. Maafisa wa ngazi za juu wa Marekani na…
Trump aikosoa Ukraine baada ya mazungumzo na Urusi
Rais wa Marekani, Donald Trump, ameikosoa Ukraine kufuatia kauli ya Rais Volodymyr Zelensky, aliyeeleza kushangazwa na kutohusishwa kwa nchi yake katika mazungumzo ya amani yaliyofanyika Saudi Arabia. Mazungumzo hayo yalilenga kutafuta suluhisho la kumaliza vita vya Ukraine vilivyoanza karibu miaka…
Papa ashindwa kuongoza misa
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, jana Jumapili ameshindwa kuongoza misa kama ilivyo kawaida yake kutokana na matatizo ya kiafya yanayomsumbua. Vatican ilithibitisha kupitia taarifa rasmi kwamba Papa Francis hatokuwa na uwezo wa kuongoza misa hiyo kutokana na changamoto…
Imamu aliyejitangaza kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja auawa
Muhsin Hendricks, mtu mashuhuri aliyejulikana kama imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameuwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 57 alikuwa anaongoza msikiti mmoja katika jijini la…





