Category: MCHANGANYIKO
Yah: Tusichezee lugha yetu, wengine wanajuta
Wakati tunatawaliwa, wakoloni wote kwa awamu zao yaani Wajerumani, Waingereza na hata Wareno na Waarabu, wakati wakipita kwa biashara zao sisi Wazaramo na Wandengereko tulikuwa tunawasiliana kwa shida sana. Kuna wakati tulikuwa tunatumia lugha ya alama kuwasiliana. Baada ya kuanza…
NUKUU
Mwalimu Nyerere: Tudhibiti tofauti za maskini, matajiri “Tofauti kati ya watu maskini na watu matajiri zinaongezeka Tanzania. Inafaa tuwe macho. …lazima tuendelee kutumia Sheria za Nchi, na mipango mbalimbali ya Serikali, kuona kuwa tofauti hizi hazifikii kiasi cha kuhatarisha umoja…
Mwadui ni bora kuliko nyingine nchini – Julio
Kocha wa Timu ya Soka ya Mwadui ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ametamba kwamba timu hiyo itakuwa bora katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuliko zote zinazoshiriki.
Akizungumza na JAMHURI hivi karibuni, Julio amesema kuwa timu hiyo itatoa upinzani mkali kwa timu za Simba, Yanga na Azam FC.
“Simba na Yanga hakuna mpira pale bali kuna makelele, niliwahi kufundisha timu ya Kajumulo, sikuwahi kufungwa na Simba wala Yanga na hata sasa nikifanya usajili wangu hakuna timu ya kunifunga kati ya timu hizo,” amesema Julio na kuongeza:
Marijani Rajabu: Jabali la Muziki lililozimika ghafla
Marijani Rajabu kweli hatunaye tena hapa duniani, lakini kamwe wadau na wapenzi wa muziki wa dansi hapa nchini hawatamsahau.
Alikuwa miongoni mwa wanamuziki waliotoa mchango mkubwa wa maendeleo ya nchi kupitia tungo za nyimbo zake maridhawa, zilizokuwa zikiendana na wakati.
Machi 23, 2014 Marijani alitimiza miaka 18 tangu atangulie mbele ya haki. Nguli huyo alifariki Machi 23, 1995 na kuzikwa siku iliyofuata katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Marijani alizaliwa Machi 3, 1955, Kariakoo, Dar es Salaam. Kwa mapenzi yake Mungu, akamchukua akiwa na umri wa miaka 40.
Hofu yatanda Katiba mpya
*Ananilea: Rais akipenda ataokoa jahazi Wingu zito limetanda juu ya mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya viongozi wa dini na wanaharakati kutabiri kifo chake. Baadhi wamekosoa mfumo wa Bunge Maalum la Katiba, na…
Vibwanga vya Waziri Lazaro Nyalandu
*Madudu yake yanamchafua Rais Kikwete
Mara tu baada ya mawaziri wanne kujiuzulu na wengine kuondolewa kutokana na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza, mwandishi mmoja aliandika makala iliyokuwa inasomeka, “Kikwete ana mkosi gani na mawaziri wake?”