Category: MCHANGANYIKO
CCM iwabaini, iwatimue wanaoihujumu
Jumatano iliyopita, baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kata mbili za Azimio wilayani Temeke na Tandale, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, waliandamana ili kupinga hujuma walizodai zinavuruga uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho na jumuiya zake zote unaoendelea hivi sasa.
Nidhamu itawapa wabunge heshima
WIKI hii tumeshuhudia michango mbalimbali ikitoka kwa wabunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Yametokea malumbano kati ya wabunge kadhaa na kiti cha Spika. Binafsi nilishuhudia tukio hili, hadi Mwenyekiti wa Bunge aliyekuwa amekalia kati cha Spika akaamuru mbunge mmoja kuondolewa ukumbini. Mabaunsa sita, walikwishajongea kwa nia ya kumtoa ukumbini, lakini yeye akajitoa mwenyewe.
Lundenga: Miss Tanzania imeitangaza nchi
Kwa muda wa miaka 18 iliyopita, mashindano ya Mrembo wa Tanzania yamekuza utamaduni, utalii na uwekezaji wa kigeni. Si hilo tu, mashindano haya yamewapa fursa mpya ya kujitambua wasichana Watanzania, anasema mwandaaji wa mashindano hayo, Hashim Lundenga.
Chadema sasa wadai rasmi Serikali ya Tanganyika
Hii ni sehemu ya maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Tundu Lissu kuhusu Mpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013. Endelea
Katika maoni yetu kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilionyesha jinsi ambavyo “tafsiri hii mpya ya Makubaliano ya Muungano na Katiba ya Jamhuri ya Muungano imetiliwa nguvu kubwa na Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo imeipa Zanzibar nafasi na ushawishi mkubwa katika utungaji wa Katiba Mpya.”
Waislamu, Walokole pigeni moyo konde
Kwa karibu miaka miwili sasa nimejiepusha kuandika mada zinazohusiana na masuala ya dini, hasa Uislamu. Niliacha kuandika si kwa sababu nyingine bali kujipa muda niweze kupima upepo, kuangalia mustakabali wa taifa hili na hatimaye kuwa na mawazo muwali yatakayoniwezesha kutoa…
Balotelli aichanganya Italia
…Ageuka pia kuwa shujaa barani Afrika
Mapema mwaka huu, Mario Balotelli aliachwa katika timu ya taifa ya Italia (Azzurri) iliyocheza na Marekani Jumamosi, Februari 29, lakini Alhamisi iliyopita ghafla aliichanganya Italia alipoipeleka kucheza mechi ya fainali za Euro 2012 hapo juzi, Jumapili, dhidi ya Hispania mjini hapa.
Habari mpya
- Rais Samia, Mwinyi, Karume wajumuika kwenye iftar Zanzibar
- Kamati ya Kudumu ya Bunge yapongeza ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishatu Mtumba
- Rais Samia kuanza ziara ya kikazi Namibia kesho
- Rais Dk Samia akutana na mjumbe maalum wa rais wa Misri
- NIT mbioni kuanzisha chuo cha mafunzo ya urubani nchini
- Zaidi ya leseni 1,000 za madini zatolewa Kahama
- Mringo ataja changamoto nne zinazowakabili wamiliki wa vyuo binafsi vya ufundi stadi
- NACTVET yawahakikishia wadau usimamizi thabiti wa ubora wa elimu ya ufundi na amali
- ALAT yawataka madiwani kuwaelezea wananchi yaliyofanywa na Dkt. Samia
- PBZ kuanza kufanyakazi kwa saa 24
- Kamati ya PAC yatembelea mradi wa kufua umeme wa Kikuletwa Hai
- TIB imezalisha ajira 12,547 kupitia uwekezaji wa miradi ya maendeleo
- Wananchi wakumbushwa matumizi sahihi ya alama za taifa
- CRDB waeleza mafanikio ya huduma za Al Barakh Songea
- Mbunge wa Viti Maalum Jackline aiomba Serikali kupitia TANROADS kuharakisha ujenzi barabara Mtwara corridor