WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameiagiza Mikoa na Halmashauri kutengeneza mikakati ya kuhakikisha masoko katika maeneo yao yanakuwa safi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akishiriki zoezi la usafi katika soko la Bonanza lililopo Jijini Dodoma zoezi lililoratibiwa na Mabalozi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma leo Julai 30,2022.

Dkt. Jafo ametoa maagizo hayo leo Julai 30,2022 wakati akishiriki zoezi la usafi katika soko la Bonanza lililopo Jijini Dodoma zoezi lililoratibiwa na Mabalozi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma.

Waziri Jafo amesema miji na masoko mengi ni machafu kwa kuwa viongozi katika maeneo hayo hawaratibu vizuri zoezi la usafi.

”Naagiza kila Mikoa na Halmashauri kutengeneza mikakati ya kuhakikisha masoko katika maeneo yao yanakuwa safi pamoja na kuratibu upatikanaji wa vifaa vya kuwekea taka katika miji yao ili kuweka mazingira yao kuwa safi.”amesema Dk.Jafo

Aidha Waziri Jafo amewapongeza abalozi wa mazingira,wafanyabiashara sokoni la Bonaza na wananchi kwa ujumla kwa kujitokeza kushiriki kufanya usafi wa mazingira.

Amewataka wafanyabiashara wa soko hilo kuendelea kudumisha kwa vitendo kampeni ya usafi na mazingira kwa ujumla.

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma mara baada kushiriki zoezi la usafi katika soko la Bonanza lililopo Jijini Dodoma zoezi lililoratibiwa na Mabalozi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma leo Julai 30,2022.

“Ndugu zangu agenda ya mazingira ni endelevu sote yatupasa kuitekeleza kwa vitendo na uwe ni utamaduni wetu sote” amesisitiza Dk. Jafo

Aidha, Waziri Jafo amesema kuwa Serikali inatarajia kuzindua Kampeni ya usafi wa mazingira itakayofahamika kama ‘My Dustbin’ kwenye mitaa ya mbalimbali nchi nzima.

Amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuweka mitaa katika hali ya usafi kwa kuwa kila mwananchi anatakiwa kutupa taka kwenye mapipa yaliyoyopo kwenye mitaa badala ya kutupa ovyo.

Aidha Mhe. Dkt. Jafo amemtaka Meneja wa DUWASA ndani ya siku 14 kuhakikisha anafanyia marekebisho ya mfumo wa maji taka katika soko hilo ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

“Ukarabati huu wa Mfumo wa maji taka katika eneo hili ufanyike mara moja, Mkurugenzi wa DUWASA asimamie kwa karibu utekelezaji wake” amesema Dk.Jafo.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dickson Kimaro amesema Jiji la Dodoma tayari limeweka utaratibu wa ufanyaji usafi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ,Dkt. Selemani Jafo akibeba taka na kuzipeleka katika vyombo maalumu vya kuhifadhi taka mara baada ya kushiriki zoezi la usafi katika soko la Bonanza lililopo Jijini Dodoma zoezi lililoratibiwa na Mabalozi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma leo Julai 30,2

”Katika soko hilo wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakijitokeza kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira sokoni hapo hivyo kuliweka jiji katika hali ya usafi”amesema Kimaro

Naye mwakilishi wa Mabalozi wa Mazingira Emanuel Likuda amesema wamekuwa wakihamasisha jamii katika kushiriki kutunza mazingira pamoja na kufanya usafi katika jiji la Dodoma.

By Jamhuri