Category: MCHANGANYIKO
RC Arusha anaendekeza ujinga dhidi ya Lema
Miaka miwili iliyopita Rais Jakaya Kikwete alipofanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, nilifurahi. Nilifurahi baada ya kusikia wamo vijana walioteuliwa, na hasa mmoja tuliyekuwa tukifanya kazi wote chumba cha habari Majira, Fatma Mwassa. Huyu sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora na anaendelea vyema.
Mchezo wa vinyoya unaweza kuibeba Tanzania Olympics
Hatimaye wadau wamejitolea kuufufua mchezo wa vinyoya, uliopoteza hadhi yake licha ya kuitangaza Tanzania kimataifa miaka ya 1960 na 1970.
Yah: Laiti lingepigwa baragumu wafu wafufuke
Kuna wakati huwa naona kama ndoto ninapowakumbuka baadhi ya watu. Namkumbuka sana marehemu baba yangu, kwa mtazamo wake na uamuzi wa kifamilia kwa wakati ule. Naona jinsi alivyokuwa na mtazamo wa kitaifa zaidi na si kifamilia.
Tumeacha kuheshimu sheria, tumekwisha
Na Deodatus Balile, Johannesburg
Wiki hii nimekuwa hapa jijini Johannesburg. Nimekuja hapa Afrika Kusini kwa nia ya kumuona Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda, aliyetekwa, akapigwa, akaumizwa, akatobolewa jicho, akang’olewa meno na kucha. Ametiwa ulemavu wa kudumu. Ni masikitiko makubwa.
Ras Inno kuitambulisha bendi yake
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, mwanamuziki nguli wa miondoko ya reggae hapa nchini, Ras Inno Nganyagwa, anarudi tena jukwaani kwa kuitambulisha rasmi bendi yake.
Yah: Bomu la elimu duni, ajira, njaa
Wiki jana nilikumbuka baadhi ya mabomu mabaya zaidi duniani, ambayo Tanzania pia tunajitahidi kuyatengeneza japokuwa mataifa makubwa yanayotengeneza silaha kali, hayataki kuja kutuchunguza ili tuwekewe vizingiti vya kiuchumi.