JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Vigogo watafuna nchi

*Wabunge wawili CCM walipwa fidia Sh milioni 964 bado jengo lauzwa
*Zitto asema kalinunua Fida Hussein
*Ataka Katibu Mkuu Fedha ahojiwe

Wakati Rais Jakaya Kikwete amebadili Baraza la Mawaziri kutokana na shinikizo la Bunge, taarifa zimevuja kutoka serikalini kuwa kuna vigogo na watendaji wakuu wanaouza mali za umma kama zao.

Orodha vigogo waliokalia kuti kavu yaanza kuvuja

[caption id="attachment_58" align="alignleft" width="139"]KikweteRais Jakaya Kikwete[/caption]Ikulu imeanza kuorodhesha watumishi wa umma wanaopaswa kufukuzwa kazi na kufunguliwa mashitaka, kutokana na kuhusishwa na ufujaji fedha za umma kama ulivyoainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Takukuru inajipendekeza kwa Rais Kikwete?

“Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu (ili) tuanze kuyashughulikia haraka,” anasema Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah.

Kuhujumu gazeti: Waingereza wangecheka hadi wafe

Zilipokuja habari za gazeti hili makini kuhujumiwa kwa nakala zote hili kununuliwa, watu wa hapa hawakuamini. Nilikuwa kwenye kijiwe cha kuvuta sigara – si unajua kila eneo la kazi pametengwa eneo la kupunguzia baridi – nilipozisikia.

Tanzania kuimarisha usambazaji wa maji jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Christopher Sayi, amesema Serikali imeanzisha mradi mkubwa wa maji katika Jiji la Dar es Salaam na utakapokamilika, kwa miaka 15 ijayo Jiji hili halitakuwa na shida ya maji.

Mkono: Hata JK yapo ya Chadema anayoyakubali

*Aeleza sababu za kusaini kumng’oa Waziri Mkuu
*Asukumwa na wizi uliofanywa mgodini Buhemba

Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM), ameamua kueleza sababu zilizomfanya asaini fomu ya majina ya wabunge katika kusudio la kumpigia kura Waziri Mkuu Mizengo Pinda ya kutokuwa na imani naye.