JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Biashara

Rushwa yazigonganisha Mahakama, Wizara

Wizara ya Nishati na Madini imeingia kwenye mvutano na Mahakama baada ya mhimili huo kuamuru raia wa China aliyekamatwa akitorosha madini ya tanzanite, arejeshewe madini hayo kinyume cha sheria.

DECI mpya yaibuka Dar

Kituo cha Mafunzo ya Ujasiriamali Tanzania kilichopo jijini Dar es Salaam, kimeingia katika kashfa ya kuwatapeli wajasiriamali walioshiriki katika semina  za ufugaji kwa kuwapa ahadi hewa.

CIDTF: Korosho inaweza kuwainua wakulima

Korosho ni moja ya mazao makuu ya biashara nchini. Kwa sasa zao hili hulimwa zaidi mikoa ya Kusini mwa Tanzania, yaani Lindi na Mtwara ikifuatiwa na Mkoa wa Ruvuma, Pwani na Tanga.

Edwin Butcher: Hatuhusiani na Dk. Amani

Mmiliki wa duka la nyama linaloitwa Edwin Butcher la Rwamishenye, Bukoba, amejitokeza na kusema kuwa bucha yake haina uhusiano wowote na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Bukoba, Dk. Anatory Amani, au udini kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.

Mapapa wa ‘unga’ watajwa

*Kinondoni, Magomeni, Mbezi, Tanga watia fora

*Wamo Wakenya, Wanigeria, waimba taarab Dar

*Wengine wapata dhamana kimizengwe, watoroka

Vita dhidi ya wauzaji na wasafirishaji dawa za kulevya inazidi kupamba moto, na sasa JAMHURI imepata orodha ya watu wengine 245 wanaotajwa kuwa ndiyo ‘mapapa’ wa biashara hiyo haramu hapa nchini.

Wauza unga 250 nchini watajwa

*Soma orodha uone maajabu, wamo masheikh, wachungaji

*Wengi wanatoka Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, Morogoro

*Mahakama yawaweka chini ya uangalizi, wanaripoti polisi

Majina ya Watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamejulikana, na JAMHURI imeamua kuyachapisha. Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wamo watu maarufu na baadhi wamekuwa wakitoa misaada, huku wengine wakijifanya ni wazee wa kanisa na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.